Yanga inaendelea na mazoezi Avic Town kujiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba utakaopigwa Jumapili, Novemba 05 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Huu ni mchezo muhimu sana kwa Yanga kwani alama tatu zitawahakikishia Wananchi wanabaki kileleni mwa msimamo wa ligi
Baada ya kupoteza mechi mbili zilizopita dhidi ya Simba, Wananchi hawako tayari kuona wanapoteza mchezo mwingine mbele ya mtani zao
Katika historia, Yanga inaongoza kwa kuifunga Simba mara nyingi kuliko timu yoyote na Wananchi hawana kawaida ya kuwa 'wateja' wa kupoteza mechi mfululizo dhidi ya Simba
Wakati mazoezi makali yakiendelea Avic Town, ni wazi kocha mkuu wa Yanga Miguel Gamondi anakuna kichwa vile atakipanga kikosi chake hasa eneo la ushambuliaji
Kwa sasa Yanga inategemea zaidi viungo washambuliaji kufunga mabao, ufanisi umekuwa mdogo kwa washambuliaji
Kennedy Musonda na Hafiz Konkoni kila mmoja amefunga bao moja tu wakati Clement Mzize bado hajafanikiwa kuzifumania nyavu kwenye ligi msimu huu
Katika mchezo uliopita dhidi ya Singida BS, Gamondi alianza na Konkoni na baadae akawaingiza Musonda na Mzize
Kuna uwezekano mkubwa Konkoni au Mzize mmoja kati yao atapewa nafasi ya kuanza katika mchezo dhidi ya Simba kwani Musonda anaonekana kutokuwa fit kwa asilimia 100 akitokea kwenye majeraha