Licha ya kuwa bado ana zadi ya miezi sita kwenye mkataba wake na Yanga, mabingwa hao wa nchi wako mbioni kumsainisha mkataba mpya kiungo mshambuliaji Stephane Aziz Ki
Moto alioanza nao Aziz Ki msimu huu umewafanya mabosi wa Yanga waharakishe mazungumzo ya kumuongezea mkataba mwingine wa miaka miwili kabla ya mkataba wake wa sasa kufikia tamati mwishoni mwa msimu
Aziz Ki ndiye kinara wa mabao katika ligi kuu ya NBC msimu huu akifunga mabao sita sawa na Jean Baleke wa Simba. Aziz Ki pia ana pasi moja ya bao
Katika kikosi cha Miguel Gamondi, Aziz Ki ndiye kiongozi kwenye safu ya ushambuliaji. Mara kadhaa Gamondi amemsifu Aziz Ki akibainisha kuwa ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa ambaye Yanga wamekuwa na bahati kuwa nae
Ni wazi kwa kiwango ambacho Aziz Ki ameonyesha mpaka sasa, yangekuwa makosa makubwa kwa uongozi wa Yanga kusubiri mkataba wake umalizike
Kuna timu zinamtolea macho! Azam Fc wameonyesha wako tayari kuingia tena vitani kusajili silaha za Yanga!
Baada ya kuwasajili Feisal Salum, Yannick Bangala na Djuma Shabani ni wazi wanamtupia macho Aziz Ki aliyewafunga mabao manne katika misimu miwili