Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema anaamini mchezo wa dabi siku ya Jumapili dhidi ya Simba utakuwa bora na mashabiki wa soka watapata burudani ya aina yake
Simba na Yanga zinachuana katika mchezo wa kwanza wa ligi kuu msimu huu ukiwa ni mchezo wa pili timu hizo kukutana bada ya Ngao ya Jamii ambao Simba walishinda kwa mikwaju ya penati
Gamondi amesema anafahamu wanakwenda kucheza na timu ngumu lakini mazingira ya mchezo huo yanampa imani kwa timu yake kupata matokeo mazuri
"Tunacheza dhidi ya timu nzuri sana yenye uzoefu katika uwanja mzuri hivyo tutacheza kadiri ya uwezo wetu ili kuhakikisha tunapata alama tatu"
"Tunawaheshimu sana wapinzani wetu na tunajua nini tunapaswa kufanya ili kushinda mchezo huo. Nafikiri ndani ya uwanja ni historia nyingine, tunafahamu tulicheza nao mwanzo wa msimu katika uwanja ambao sio rafiki ambao haukuruhusu kucheza vile tulihitaji na pengine ilikuwa hivyo hata kwa wapinzani wetu"
"Nafikiri mchezo ujao siku ya Jumapili utakuwa bora kuutazama na kuufurahia kwa timu zote mbili na mashabiki wa soka Tanzania," alisema Gamondi