Walinzi wa Yanga Dickson Job na Ibrahim Bacca wamewataka mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi uwanja wa Benjamin Mkapa siku ya Jumapili Novemba 05 katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba
Job amesema wanafanya maandalizi ya uhakika ili kuhakikisha wanapata matokeo mazuri katika mchezo huo utakaopigwa saa 11 jioni

"Yule atakayejiandaa vizuri ndiye atakuwa na nafasi kubwa ya kushinda mchezo hivyo sisi tunafanya maandalizi mazuri, tunawaomba mashabiki wetu waje kwa wingi uwanjani kutuunga mkono kwani wingi wao utatuongezea morali ya kupambana na kupata matokeo mazuri katika mchezo huo"
"Kama mchezaji siwezi kusema tutashinda ngapi au tutafungwa lakini ninachowaahidi mashabiki ni kuwa sisi tutakwenda kupambana kwa dakika zote 90," alisema Job
Nae Bacca amesema alama tatu ndio matokeo wanayohitaji zaidi kama wachezaji, amewataka mashabiki wajitokeze kwa wingi siku hiyo
"Tunaendelea vizuri na maandalizi, mwalimu anaendelea kutupatia mbinu na maelekezo ambayo yatatusaidia kupata ushindi katika mchezo huo"
"Mchezo utakuwa mgumu hilo liko wazi kwa sababu ni derby lakini sisi hatuna hofu yoyote tukiamini maandalizi tunayofanya yatatupa nafasi ya kufanya vizuri"
"Tunawaomba mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi keshokutwa kutushangilia, wingi wao utatuongezea morali ya kupambana na kushinda mchezo huo"
Yanga imejichimbia Avic Town kwa wiki nzima ikijiandaa na mchezo huo ambapo safari hii hakuna tambo nyingi kutoka kwa Wananchi
Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amesema tambo za Wananchi zitaanza baada ya dakika 90 za mchezo huo, kwa sasa uongozi unahakikisha timu inapata mazingira mazuri ya maandalizi ya mchezo huo