Msemaji wa zamani wa klabu ya Yanga Haji Manara amesema pamoja na tambo za Simba kuelekea mchezo wa kwanza wa derby kwenye ligi kuu msimu huu, mchezo huo hautakuwa mwepesi kama wanavyofikiria
Manara amesema mara nyingi mechi hizi za derby hazitabiriki, timu itakayokuwa imefanya maandalizi mazuri na kucheza kwa nidhamu katika mchezo itakuwa na nafasi ya kuibuka na ushindi
"Nimewasikia baadhi ya viongozi na hata wachezaji wao wakitamba kuwa wanakwenda kutufunga Jumapili"
"Nilibahatika kutazama mahojiano ya Kibu Denis akitamba kuwa 'alitukanda' na anakwenda 'kutukanda' tena. Kama anadhani itakuwa rahisi basi anajidanganya"
"Hizi tambo inafaa tuwaachie wasemaji wa klabu na mashabiki lakini sio wachezaji. Kama alibahatisha kufunga mchezo uliopita, asidhani itakuwa rahisi tena. Nimwambie tu, hizi clip zao sisi tunawaonyesha wachezaji wetu, halafu sasa shughuli wataiona siku ya Jumapili," alisema Manara
Yanga imeendelea na maandalizi yake 'kimya-kimya' Avic Town kuelekea mchezo huo ambao Wananchi wanazihitaji alama zote tatu ili kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi