Mvua imeendelea kunyesha jijini Dar es salaam saa chache kabla ya mchezo wa ligi kuu ya NBC kati ya Simba dhidi ya Yanga ambao utapigwa saa 11 jioni katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Mashabiki wanaendelea kumiminika uwanja wa Benjamin Mkapa kushuhudia mchezo huo pasipo kujali changamoto ya mvua
Bodi ya Ligi imesisitiza kuwa leo mchezo utachezwa kama ulivyopangwa!
Hivyo Wananchi twende kwa wingi dimba la Mkapa kuongeza hamasa kwa wachezaji kuelekea mchezo huo
Yanga imefanya maandalizi kucheza katika mazingira yoyote, na hii haitakuwa mara ya kwanza Wananchi kucheza katika mvua
Itakuwa vita ya dakika 90 ndani ya uwanja wa Benjamin Mkapa
ADVERTISE HERE