Unakumbuka ahadi iliyotolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Paul Makonda kuwa kila goli la mchezo kati ya Simba dhidi ya Yanga litanunuliwa kwa n'gombe mmoja?
Kuna n'gombe watano watachinjwa pale Jangwani siku ya Jumapili na Wananchi kunywa supu
Ni kufuatia ushindi wa mabao 5-1 ambao Yanga aliupata dhidi ya watani zao Simba
Meneja wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amewaalika Wananchi Jangwani siku ya Jumapili
"Tunawaambia Wanayanga siku ya Jumapili kila mmoja aje pale Jangwani na chapati, maandazi, vitumbua, pilipili na vinginevyo, supu tutaitoa sisi bure kabisa..!," alitamba Kamwe
Wananchi bado wako kwenye kilele cha furaha kufuatia ushindi wa kihistoria dhidi ya Simba huku timu yao ikiendelea kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya ushindi dhidi ya Coastal Union