Wakati ligi kuu ya NBC ikisimama, Yanga inakwenda kwenye mapumziko ya Kimataifa ikiwa katika nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi
Unaweza kusema baada ya mechi tisa, maji na mafuta yameanza kujitenga kwani kila timu iko katika nafasi yake!
Yanga imeshinda mechi nane kati ya tisa walizocheza na kufikisha alama 24. Hakuna timu iliyoshinda mechi nyingi kuliko Wananchi msimu huu
Azam Fc na Simba zinafuatia kama ilivyo kwenye msimamo kila moja ikiwa imeshinda mechi sita
Mpaka sasa Wananchi wanaongoza katika takwimu zote muhimu, Yanga ndio timu iliyofunga mabao mengi kuliko nyingine zote (26) huku Wananchi pia wakiwa timu iliyofungwa mabao machache (5)
Uwiano wake wa mabao 21 ni tofauti ya mabao 11 dhidi ya Azam Fc iliyo nafasi ya pili na mabao 14 dhidi ya Simba iliyo nafasi ya tatu
Kwa hakika vijana wa Miguel Gamondi kama wataendeleza kasi hii, wanaweza kutangaza ubingwa mapema sana msimu huu
