Mwanzoni mwa msimu huu, beki wa zamani wa Yanga Abdallah Shaibu 'Ninja' alisajiliwa na klabu ya Fc Lubumbashi Sport inayoshiriki Ligi Kuu ya DR Congo
Katika muda mfupi aliyoitumikia timu hiyo, Ninja amejihakikishia nafasi kwenye kikosi cha kwanza
Kiwango chake bora kimemfanya aorodheshwe kwenye kikosi bora cha nusu msimu Ligi kuu nchini DR Congo
Ninja aliondoka Yanga mwishoni mwa msimu uliopita akiwa mchezaji huru baada ya mkataba wake kumalizika
Awamu yake ya pili baada ya kurejea Yanga haikuwa na mafanikio kutokana na kukabiliwa na mfululizo wa majeraha
Uongozi wa Yanga ulifanya jitihada za kumtibia majeraha hayo ikiwa ni pamoja na kumpelekea Tunisia kufanyiwa matibabu ya goti
Sasa amerejea katika ubora wake baada ya kupona majeraha
ADVERTISE HERE