Mambo ni magumu kwa Konkoni

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Nov 2023
Mambo ni magumu kwa Konkoni

Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amethibitisha kuwa kwenye dirisha dogo ambalo litafunguliwa Disemba 15, kutakuwa na maingizo mapya kwa ajili ya kuboresha maeneo yenye changamoto

Tayari Yanga kwa kushirikiana na benchi la ufundi wamebaini nafasi zinazohitaji kuboreshwa, safu ya ushambuliaji na kiungo ni miongoni

Mshambuliaji Hafiz Konkoni yuko katika wakati mgumu kwani ameshindwa kulishawishi benchi la ufundi

Yanga huenda ikarejea tena kwa Ranga Chivaviro ambaye walimkosa dakika za mwisho kwenye dirisha la usajili lililopita baada ya Kaizer Chiefs kuingilia

Yanga pia inasaka kiungo mkabaji ili kuongeza nguvu eneo hilo ambalo kwa sasa Mganda Khalid Aucho ndiye anayetegemewa zaidi

Katika moja ya mahojiano aliyofanya karibuni, Hersi alisema wanahitaji kufanya maboresho ili kukabiliana na changamoto ya kushiriki michuano mingi

"Hivi karibuni tunaanza hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa, tunahitaji kuongeza nguvu katika baadhi ya maeneo. Pia tunatarajia ugumu wa ratiba kutokana na ushiriki wetu kwenye michuano mbalimbali"

"Tunafanya kazi kwa ukaribu na benchi la ufundi kuhakikisha tunafanya maboresho ambayo yatakwenda kutuongezea makali zaidi," alisema

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’