Mashabiki na Wanachama wa Yanga leo walikutana Makao Makuu ya klabu hiyo katika siku iliyopewa jina la Mwananchi Supu Day
Siku hii ilikuwa na mambo mengine zaidi ya kunywa supu. Wananchi walikutana kujadili mipango yao kuelekea mechi zinazofuata hasa hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa
Mchezo wa kwanza nyumbani ni dhidi ya Al Ahly na utapigwa Disemba 02 malengo yakiwa kushinda mchezo huo pamoja na mingine yote itakayopigwa kwa Mkapa
Mashabiki pia wakapata nafasi ya kusajiliwa kuwa Wanachama au Mashabiki wanaotambulika pamoja na wenye kadi kulipia ada zao
Aidha Mkurugenzi wa Sheria wa Yanga Simon Patrick amesema leo imezinduliwa rasmi ofa yenye punguzo la bei ya viingilio kwa Wanachama wenye kadi 'hai'
"Tumezindua ofa kwa wanachama kuelekea mechi zetu za kimataifa; wanachama waliojisajili na kulipa ada watapata punguzo la 50% kwenye tiketi zote"
"Hii inamaanisha VIP A - 50,000 mwanachama atalipia 25,000, VIP B - 30,000 mwanachama atalipia 15,000, VIP C - 20,000 mwanachama atalipia 10,000, jukwaa la rangi ya chungwa 10,000 mwanachama atalipia 5000, na mzunguko 5000 mwanachama atalipia 2500"


