Yanga itawashangaza wengi CAF CL - Arafat

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Nov 2023
Yanga itawashangaza wengi CAF CL - Arafat

Makamu wa Rais wa Yanga Arafat Haji amesema wamejipanga kufuta unyonge dhidi ya timu za Kaskazini mwa Bara la Afrika kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa hatua ya makundi

Yanga iliyopangwa kundi D, itacheza mechi nne dhidi ya CR Belouizdad (Algeria) na Al Ahly (Misri) kwenye hatua ya makundi katika kundi ambalo pia wamo mabingwa wa Ghana, Medeama

"Kwa muda mrefu mashindano ya Afrika (CAF Champions League na CAF Confederation Cup) yamekuwa yakitawaliwa na timu za Kaskazini mwa Afrika. Yanga kukutana na timu mbili kwenye hatua ya makundi kutoka ukanda wa Kaskazini mwa Afrika (Al Ahly na CR Belouizdad) inatupa fursa ya kucheza na timu zenye uzoefu"

"Endapo tutatoka kwenye kundi hilo tutakuwa tumepata mechi zenye ushindani mkubwa. Kwa ubora wa kikosi chetu, tunaamini tutavuka hatua ya makundi na kwenda hatua inayofuata na safari yetu itaendelea hadi hatua ambayo hakuna timu ya Tanzania iliyowahi kufika kwenye mashindano haya ya Ligi ya mabingwa Afrika," alisema Arafat

Arafat mafanikio ambayo yameanza kupatikana sasa, yametokana na uwekezaji mkubwa uliofanyika baada ya timu kutoka kwenye kipindi kigumu. Amesema dhamira yao ni kufanya zaidi ya kuhakikisha Yanga inakuwa moja ya klabu zenye heshima kubwa kwenye soka la Afrika

"Yanga ilipitia kipindi kigumu sana mwaka 2018-2019, nafikiri lile lilikuwa ni fundisho kubwa ambalo limetusaidia kujipanga upya na mafanikio ambayo tumetapata hayajatokea kwa bahati mbaya. Ni matunda ya mipango na mikakati ambayo tulijiwekea katika kuhakikisha tunaivusha timu na kuifikisha mbali"

"Kwetu ni furaha na faraja kubwa kuona timu yetu imetoa wachezaji wengi wanaowania tuzo za CAF kwa mashindano ya msimu uliopita. Mafanikio ya Yanga ni mafanikio ya Tanzania, ndio maana Yanga inatoa wachezaji wengi kwenye timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, kwa hiyo huwezi kuitengenisha Yanga na mafanikio ya timu ya Taifa"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
6m ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
46m ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
4h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
23h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’