Gamondi ataka mechi kabla ya kwenda Algeria

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Nov 2023
Gamondi ataka mechi kabla ya kwenda Algeria

Kikosi cha Yanga kinaendelea na mazoezi Avic Town kujiandaa na mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya CR Belouizdad

Wananchi watasafiri kwenda Algeria ambapo Novemba 24, kwenye Uwanja wa 5 July 1962, watakuwa wageni wa Belouizdad

Ni katika uwanja huo ambao Yanga wana kumbukumbu ya ushindi wa bao 1-0 dhidi USM Alger na kukaribia kutwaa Kombe la Shirikisho Barani Afrika kama sio kutumika sheria ya mabao ya ugenini

Kabla ya kuelekea Algeria, Gamondi amewaagiza mabosi wa Yanga kutafuta mechi moja ya kirafiki ili kuwaweka sawa wachezaji wake tayari kwa mchezo huo

Ligi ya Algeria haijasimama Belouizdad wamecheza juzi na watarajia kucheza tena Novemba 19. Mchezo wa mwisho kwa Yanga ulikuwa Novemba 08 dhidi ya Coastal Union, takribani wiki moja wamekosa mechi ya ushindani

Gamondi anaamini mechi hiyo itawaweka kwenye ushindani wachezaji ambao hawana majukumu ya timu za Taifa kwani wale ambao wako kwenye timu za Taifa wengi watacheza mechi za kuwania kufuzu kombe la Dunia 2026

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
10h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
14h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
15h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
15h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
20h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’