Leo saa nne usiku kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kitashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuwabakili Morocco katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za kombe la Dunia 2026
Mechi muhimu sana kwa Tanzania kusaka ushindi nyumban ili kuweka hai matumaini ya kusaka tiketi ya kombe la Dunia
Nyota wa Yanga Bakari Nondo Mwamnyeto, Ibrahim Hamad Bacca na Dickson Job wanaunda safu ya ulinzi ya Stars, leo watakuwa na kazi kuhakikisha lango la Stars linakuwa salama kabla ya kuelekea Algeria kuungana na wenzao ambao wameondoka nchini Alfajiri ya leo
Ijumaa, Novemba 24 Yanga itakabiliana na CR Belouizdad katika mchezo wa kwanza hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika
Walinzi hao leo wanakabiliana na timu bora barani Afrika ambayo mwaka uliopita iliweka rekodi ya kuwa Taifa la kwanza la Afrika kucheza nusu fanali ya kombe la Dunia
Mchezo wa leo utakuwa maandalizi mazuri kwao kuelekea mchezo dhidi ya CR Belouizdad ambao unawasubiri siku ya Ijumaa
Baada ya mchezo huo nyota wa Yanga hawatakuwa na muda wa kupumzika kwani watapaswa kusafiri kuelekea Algeria usiku wa leo