Kundi la kwanza la kikosi cha Yanga limewasili jana nchini Algeria tayari kuikabili CR Belouizdad katika mchezo wa kwanza hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika
Yanga ilikuwa ifikie hoteli moja ya kisasa yenye hadhi ya nyota nne lakini baadae uongozi ukaamua kurudi hoteli Legacy Luxury ambayo walifikia msimu uliopita kwenye mchezo wa fanali CAF CC dhidi ya USM Alger
Yanga ina kumbukumbu ya kufanyiwa vurugu na mashabiki wa USM Alger usiku wa kuamkia mchezo wa fainali. Shirikisho la soka Afrika (CAF) lilitoa onyo kwa klabu ya USMA na chama cha soka cha Algeria kutokana na matukio hayo ambayo yalipelekea USMA kupigwa faini
Kutokana na onyo ni wazi Shirikisho la Algeria na CR Belouizdad watakuwa na wajibu wa kudhibiti mashabiki wao kwani kinyume na hivyo kama watarejea tena matukio waliyofanya msimu uliopita, watakumbana na adhabu kali zaidi
Uongozi wa Yanga umehakikisha wachezaji wanapata utulivu, timu imepata mapokezi mazuri na leo inatarajiwa wachezaji wote waliokuwa na majukumu ya timu za Taifa watawasili