Kiungo mshambuliaji wa Yanga Skudu Makudubela amesema jezi zilizozinduliwa na Yanga jana ambazo zitatumika kwenye michuano ya ligi ya mabingwa, zitawaongezea morali wachezaji wajihisi wana deni kubwa
Skudu raia wa Afrika Kusini amekiri kuwa ni mara ya kwanza kushuhudia ubunifu wa aina yake katika jezi za timu ya mpira wa miguu
"Nahisi kulia kwani sijawahi kuona kitu kama hiki. Majina ya wachezaji kuwemo ndani ya jezi, ina maana kubwa sana, ni heshima kwa wachezaji"
"Siku zote watu wanasema cheza kwa ajili ya nembo ya timu lakini hapa sasa hata jina lako liko kwenye jezi hii"
"Hii ni zawadi kubwa, dunia ni kijani na jua ni njano, jezi yenye rangi ya Ulimwengu...!," alisema Skudu
Jezi hizo zinatarajiwa kuanza kupatikana madukani Novemba 30 kwa bei ya Tsh 50,000/-Β
"I have never seen something like this. Names engraved on a jersey, IT MEANS SO MUCH MORE" #SkuduMakudubela
— Young Africans SC (@YoungAfricansSC) November 22, 2023
OFFICIAL #CAF CL
YOUNG AFRICANS SC KITS 2023/24#TimuYaWananchi #DaimaMbeleNyumaMwiko pic.twitter.com/6CDpDNGgrL