Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema kikosi kiko tayari kwa mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya CR Belouizdad ambao utapigwa leo Ijumaa katika uwanja wa Julai 05, Algeria
Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari jana, Gamondi alisema anatambua mchezo huo utakuwa mgumu lakini watacheza soka lao huku wakiwaheshimu wapinzani wao
"Tunakwenda kucheza mechi ngumu dhidi ya CR Belouizdad, sisi tuko tayari kwa mchezo huo na tutajaribu kucheza soka la kuvutia kuwapa furaha Wananchi"
"Natambua CR Belouizdad ni timu kubwa yenye wachezaji wazuri hivyo hautakuwa mchezo rahisi kwa kuzingatia changamoto za hapa na pale ambazo zimetukabili baadhi ya wachezaji wakirejea kutoka ratiba ya mechi za timu za Taifa"
"Tumekuwa na mwendelezo mzuri katika mechi zilizopita, nimewaambia wachezaji tunahitaji kupambana ili kuhakikisha tunapata matokeo mazuri katika mchezo huo," alisema Gamondi
Yanga ilikamilisha mazoezi ya mwisho jana usiku katika uwanja wa July 05 ambao mchezo huo utapigwa hii leo