Leo Yanga inaanza kampeni ya michuano ya ligi ya mabingwa (CAF CL) hatua ya makundi kwa kuikabili CR Belouizdad katika mchezo utakaopigwa saa 4 usiku, uwanja wa July 05 1962
Kwa mara ya kwanza leo Yanga itatumia jezi mpya zilizozinduliwa juzi ambazo ni maalum kwa ajili ya ligi ya mabingwa
Uzi wa kijani utavaliwa na Wananchi wakati wapinzani wao CR Belouizdad wanatarajia kuvaa jezi zao nyekundu ambazo huzitumia katika mechi zao za nyumbani
Yanga imepania kuanza vyema hatua ya makundi, ushindi au hata matokeo ya sare yatakuwa na maana kubwa kwa Wananchi
Yanga ina takwimu nzuri sana katika michuano ya CAF kwa mechi zilizopigwa ugenini ambapo tangu msimu uliopita imepoteza mechi moja tu ugenini na kutoka sare mechi moja tu na kushinda mechi sita
Bila shaka ubabe huo utaendelea Algiers baadae leo