Diarra ni majeruhi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Nov 2023
Diarra ni majeruhi

Mlinda lango Djigui Diarra jana hakuwa sehemu ya kikosi kilichoikabili CR Belouizdad katika mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa kundi D

Diarra aliushuhudia mchezo huo ambao Yanga ilikubali kipigo cha mabao 3-0 akiwa jukwaani

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema Diarra anasumbuliwa na tatizo la bega

Kamwe amesema wanatarajia atakuwa tayari kuikabili Al Ahly katika mchezo unaofuata utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa Jumamosi Disemba 02

"Diarra ana tatizo la bega. Alipata majeraha kwenye mchezo dhidi ya Simba na hata mchezo dhidi ya Coastal Union hakucheza"

"Aliitwa timu ya Taifa lakini nako hakucheza kutokana na tatizo hilo. Madaktari walishauri apate muda wa kupumzika ili kuhakikisha anapona kabisa," alisema Kamwe

Kikosi cha Yanga kitaondoka Algeria baadae leo na kitawasili nchini Alfajiri ya kesho Jumapili

Kamwe amesema baada ya timu kurejea watakuwa na muda mfupi wa mapumziko kabla ya kurejea mazoezini kuanza maandalizi ya mchezo dhidi ya Al Ahly

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’