Leo Yanga imesaini makubaliano ya udhamini wa wiki ya Bacca kuelekea Bacca Day ambayo itahitimishwa Disemba 02 katika uwanja wa Benjamin Mkapa kwa mchezo kati ya Yanga dhidi ya Al Ahly hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika
Mamlaka ya mapato ya Zanzibar (ZRA) na ZIPA kila moja zimetoa Tsh Milioni 20 kwa ajili ya kudhamini wiki ya Bacca hivyo kuifanya Yanga kuingiza Tsh Miliooni 40 katika siku tano
Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe na kitengo chake wanastahili pongezi kwa ubunifu huu ambao sasa umeanza kuingizia klabu mapato
Kamwe alianza na Maxi Day mechi ya nyumbani dhidi ya Asas Fc, ikafuatia Aziz Ki Day mechi dhidi ya Al Hilal na sasa Bacca Day mechi dhidi ya Al Ahly imepata udhamini
Utaratibu huu utaendelea kwa mechi zote za Ligi ya Mabingwa ambazo Yanga iko nyumbani
Wachezaji zaidi wataendelea kupewa thamani huku Yanga ikiendelea kuingiza fedha