Kocha Msaidizi wa zamani wa Yanga Cedric Kaze amempongeza Rais wa Yanga Injinia Hersi Said kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa kwanza wa umoja wa klabu barani Afrika (ACA)
Kaze amesema yanayotokea sasa katika maisha yake ya uongozi kwenye soka ni matokeo ya kujitolea, imani na uaminifu wake
"Hongera sana Mheshimiwa Rais, Unastahili sana kile kinachokuja mbele yako. Uongozi, Kujitolea, Imani na Uaminifu ndivyo vinakutambulisha"
"Nakutakia kheri katika jukumu lako jipya," aliandika Kaze ambaye mwanzoni mwa msimu aliinoa klabu ya Namungo Fc kabla ya kuachia ngazi baada ya mfululizo wa matokeo mabaya
Hersi alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa ACA asilimia 99 ya kura zote zilizopigwa. Anakuwa Mwenyekiti wa kwanza wa Umoja huo
ADVERTISE HERE