Baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Al Ahly, kikosi cha Yanga sasa kinaweka nguvu katika mechi mbili zinazofuata dhidi ya Medeama Fc ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutinga robo fainali
Disemba 08 Yanga itakuwa ugenini kumenyana na Medeama huko Ghana na timu hizo kurudiana jijini Dar es salaam katika uwanja wa Benjamon Mkapa, Disemba 20
Hizi ni alama sita muhimu kwa Yanga ambazo zinaweza kuweka hai matumaini ya kufuzu robo fainali
Al Ahly inaonekana kuwa timu ngumu zaidi katika kundi D, mchezo unaofuata watakuwa nyumbani kuumana na CR Belouizdad
Kimahesabu Yanga inahitaji angalau alama tisa kutoka mechi nne zilizobaki ili kuwa na nafasi nzuri ya kusonga mbele
Bado haijaisha mpaka iishe...!
ADVERTISE HERE