Jana Rais wa Yanga Eng.Hersi Ally Said alimtembelea Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nyumbani kwake na kupata nafasi ya kuvuna busara zake
Pamoja na kuongelea mambo mbalimbali ya maendeleo yanayohusu klabu ya Yanga, Dkt. Jakaya Kikwete alimpongeza Eng. Hersi kwa kuwa Mwenyekiti wa kwanza wa Shirikisho la Vilabu Afrika (ACA) na kuingia katika kamati ya utendaji ya Shirikisho la Soka barani Africa (CAF)

ADVERTISE HERE