Kiungo mshambuliaji wa Yanga Stephane Aziz Ki alizungumzwa sana baada ya mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Ahly uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa wiki iliyopita na kumalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1
Katika mchezo huo, kipindi cha pili kilikuwa kigumu kwa Aziz Ki ambaye Al Ahly walimuwekea mkakati wa kumyima nafasi na muda kila aliposhika mpira
Unaweza kusema mechi mbili za hatua ya makundi, ukianzia mchezo dhidi ya CR Belouizdad, Aziz Ki hakufikia ule ubora ambao Wananchi wameushuhudia kutoka kwake msimu huu
Kesho Ijumaa Aziz Ki ana nafasi nyingine ya kuwajibu wakosoaji wake kuwa yawezekana 'form' yake ilikuwa chini katika mechi zilizopita lakini bado yeye ni mchezaji wa daraja la juu
Mchezo dhidi ya Medeama utakuwa mgumu lakini bila shaka utakuwa mchezo wa wazi kwani Yanga inahitaji kushinda na hata Medeama watahitaji kutumia vyema uwanja wao wa nyumban kusaka ushindi
Msimu uliopita, bao alilofunga Aziz Ki katika mchezo dhidi ya Club Africain ugenini liliipeleka Yanga hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho (CAF CC)
Kesho Yanga inahitaji tena uchawi wa miguu Aziz Ki ugenini Ghana mbele ya Medeama ili kuondoka na alama zote tatu