Kazi ni moja Ghana leo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Dec 2023
Kazi ni moja Ghana leo

Jioni ya leo Yanga itakuwa uwanja wa Baba Yara katika Mji wa Kumasi kuikabili Medeama Fc katika mchezo wa ligi ya mabingwa barani Afrika, raundi ya tatu kundi D

Hii ni mechi muhimu sana kwa Yanga kuzisaka alama zote tatu huko ugenini katika mchezo ambao unatarajiwa kuwa mgumu

Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari jana, Mkufunzi wa Yanga Miguel Gamondi aliweka wazi kuwa kikosi chake leo kitashuka dimbani wakiwa na dhamira moja, kusaka ushindi

Yanga imedhamiria kutinga robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa, ili kufanikisha hilo Wananchi wanahitaji kukusanya angalau alama 9 kutoka mechi nne zilizosalia

Kama Yanga itashinda leo, itafikisha alama nne huku ikiwa na mechi mbili nyumbani ambazo kama itashinda itafikia malengo ya alama 10

Hautakuwa mchezo rahisi kwa kuwa hata Medeama Fc wana hesabu zao za kushinda mechi zote nyumbani

Walishinda mchezo uliopita dhidi ya CR Belouizdad na leo watashuka tena uwanjani kusaka ushindi wa pili

Kwa hakika zitakuwa dakika 90 za kutoka jasho jingi kwa wachezaji wa Yanga ili kuhakikisha ushindi unapatikana na kama sio ushindi basi hata sare lakini sio kupoteza mchezo

Mchezo utapigwa saa 10 jioni kwa saa za Ghana ambapo hapa Tanzania itakuwa saa 1 usiku

Kila la kheri Wananchi...!

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’