Msimu uliopita katika michuano ya kombe la Shirkisho barani Afrika (CAF CC) kiungo Salum Abubakar 'Sure Boy' alijipambanua kuwa mchezaji wa mechi muhimu
Sure Boy aling'ara katika mechi zote ambazo Yanga ilihitaji ushindi akianza na mechi ya kuwania kufuzu makundi dhidi ya Club Africain, ugenini Tunisia
Pamoja na kuwa nafasi yake kwenye kikosi cha Miguel Gamondi imekuwa finyu msimu huu, lakini Sureboy ni miongoni mwa wachezaji ambaye huzipenda mechi hizi zenye 'tension' kubwa
Pengine leo Sure boy atakuwa na dakika zake katika mchezo dhidi ya Medeama ambao utapigwa saa 1 usiku katika uwanja wa Baba Yara
Sureboy yuko 'fit' na ameonekana 'kuutaka' mchezo huo ambao Yanga inawania ushindi muhimu ugenini
Kocha Gamondi anazo silaha za kutosha kuiangamiza Medeama Fc baadae leo, ni yeye kuamua aanze na silaha zipi