Habari njema kwa Wananchi ni kurejea kikosini kwa mlinzi wa kushoto wa Yanga Joyce Lomalisa Mutambala
Lomalisa alipata majeraha katika mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Ahly uliopigwa Disemba 02 uwanja wa Benjamin Mkapa
Jana alianza mazoezi mepesi Avic Town na huenda akawa tayari kurejea uwanjani kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Medeama utakaopigwa Disemba 20
Lomalisa amekuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha kocha Miguel Gamondi na mara nyingi anapokosekana uwanjani pengo lake huonekana wazi
ADVERTISE HERE