Wachezaji 13 wa Yanga wamejumuishwa katika vikosi vya awali kwa ajili ya michuano ya Afcon 2023 itakayofanyika huko Ivory Coast mwanzani mwa mwaka 2024
Nyota hao ni Metacha Mnata, Aboutwalib Mshery, Nickson Kibabage, Dickson Job, Bakari Mwamnyeto na Ibrahim Bacca
Wengine ni Mudathir Yahya na Clement Mzize wakikamilisha idadi ya wachezaji 53 waliounda kikosi cha awali cha Stars ambacho kitachujwa na kubaki wachezaji 25
Pacome Zouzoua ameitwa kikosi cha awali cha Ivory Coast, Stephane Aziz Ki (Burkina Faso), Djigui Diarra (Mali), Hafiz Konkoni (Ghana) na Joyce Lomalisa (DR Congo)
Michuano ya Afcon 2023 inatarajiwa kuanza Januari 13 huko Ivory Coast
ADVERTISE HERE