Leo ni kumbukumbu ya kuzaliwa wachezaji wawili wa Yanga, mshambuliaji Kennedy Musonda na mlinzi wa kulia Yao Kouassi
Ifikapo Januari 2024, Musonda raia wa Zambia atatimiza mwaka mmoja tangu alipojiunga na mabingwa hao wa Tanzania Bara
Msimu huu bado hajaonyesha kile Wananchi walichokishuhudia kutoka kwake msimu uliopita hasa kwenye michuano ya kombe la Shirikisho la CAF (CAF CC)
Lakini ameendelea kufunga mabao kila anapopatiwa nafasi na kocha Miguel Gamondi. Amepachika jumla ya mabao sita katika mashindano yote
Yao amefanya maajabu makubwa tangu atue Yanga mwanzoni mwa msimu akitokea Asec Mimosas

Tunawatakia kila la kheri katika siku hii muhimu ya kuzaliwa kwao..!
ADVERTISE HERE