Baada ya kuwasili mkoani Singida jana, kikosi cha Yanga leo kinatarajia kufanya mazoezi kwenye uwanja wa Namfua ambao utatumika katika mchezo wa robo fainali kombe la FA dhidi ya Singida United.
Mchezo huo unapigwa kesho Jumapili, April 01 ikiwa ni siku ya Pasaka pia.
Yanga imetua Mjini Singida jana jioni na baada ya kufika tu, wachezaji walipewa wasaa wa kufanya matembezi maeneo mbalimbali ya mji ikiwa moja ya mbinu ya kuwafanya waizoee kwa haraka hali ya hewa ya Mji huo.
Azam TV watarusha mubashara mtanange huo utakaoanza kesho saa kumi kamili jioni.

ADVERTISE HERE