Mmetaka mshambuliaji? hesabuni siku - Kamwe

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Dec 2023
Mmetaka mshambuliaji? hesabuni siku - Kamwe

Meneja wa kitengo cha Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amesema klabu inakwenda kujibu kilio cha wale waliohitaji timu hiyo kusajili mshambuliaji lakini ametoa tahadhari usajili huo utakuja na maumivu makali kwa wapinzani

Siku chache zilizopita, Kamwe alitangaza kuwa Wananchi wana siku saba za kusubiri kabla ya utambulisho wa mshambuliaji mpya

Ni siku nne zimebaki kabla ya Yanga kumtangaza mshambuliaji huyo ambaye Kamwe aliweka bayana kuwa sio mgeni kwani wengi wanamfahamu

Kamwe amesema kwa sasa Yanga inae mchezaji kinara wa mabao katika ligi kuu ya NBC, Stephane Aziz Ki lakini kwa kuwa kuna ambao hawajatosheka na vipigo basi wanaleta mshambuliaji ili kuongeza uzito wa vipigo vyao

"Kama tunae mshambuliaji kama Aziz Ki ambae anaongoza kwa ufungaji akiwa na mabao 10 na bado mnauliza usajili wa mshambuliaji mpya, ni ishara hamridhiki na vipigo vyetu, nyie mnataka tuje tumpige mtu 8 au 9 ndio mridhike? Haya sasa hesabuni siku tunamleta huyo mshambuliaji mnaemtaka," alitamba Kamwe

Wachezaji wanaotajwa zaidi kuhusishwa na mchezaji huyo ni Simon Msuva na Moses Phiri ambaye inaelezwa yuko kwenye mchakato wa kuvunja mkataba wake na Simba

Hata hivyo huenda Yanga ikamrejesha Msuva ambaye hivi karibuni alifikia makubaliano ya kusitisha mkataba wake na JS Kabylie ya Algeria

Msuva ni mchezaji wa ndani hivyo usajili wake hautahitaji kupunguza mchezaji mwingine kama ambayo Yanga italazimika kufanya kama itasajili mchezaji wa kigeni. Ni lazima ipunguze nyota mmoja wa kigeni kwa kuwa idadi ya wachezaji 12 wa kigeni imetimia

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
18h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
21h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
22h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
23h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’