Baada ya klabu za Bandari Fc na URA kujitoa katika michuano ya kombe la Mapinduzi inayoanza Alhamisi visiwani Zanzibar, mabadiliko yamefanyika katika makundi
Kulingana na ratiba mpya iliyotolewa, klabu za JKU (Zanzibar) na Jamus Fc (Sudan Kusini) zimeongezwa kuchukua nafasi za URA na Bandari Fc
Jamus Fc imeingia kundi C ikiungana na Yanga, Jamhuri na KVZ wakati JKU imeingia kundi B lenye timu za Simba, APR na Singida BS
Bingwa wa michuano hiyo ataondoka na kitita cha Tsh Milioni 100 ikiwa ni ongezeko la Milioni 50 zaidi ya zawadi aliyopata bingwa msimu uliopita
Yanga inatarajiwa kuelekea visiwani Zanzibar Disemba 30, 2023 ambapo mchezo wa kwanza ni Disemba 31 dhidi ya Jamhuri

ADVERTISE HERE