Achana na taarifa ya kukamilika kwa usajili wa winga Augustine Okrah kutoka Ghana ambaye imeelezwa tayari yuko visiwani Zanzibar na ataungana na Yanga inayotarajiwa kuwasili visiwani humo kesho kushiriki michuano ya kombe la Mapinduzi
Yanga inahusishwa na mshambuliaji Basiala Ageee kutoka klabu ya As Maniema ya DR Congo
Baada ya usajili wa Maxi Nzengeli uliojibu mapema tu, Yanga imerudi tena Maniema na wakati huu huenda ikamn'goa Ageee
Msimu huu Ageee (25) amepachika ambao matano na kutoa assist tano hii inaonyesha ni mshambuliaji ambaye anaweza kwendana na mahitaji ya kocha Miguel Gamondi
Katika dirisha hili dogo la usajili Yanga haitarajiwi kufanya usajili mkubwa, wachezaji watakaosajiliwa ni kwa ajili ya kuimarisha maeneo yaliyoonyesha kuwa na mapungufu
Safu ya ushambuliaji na winga ndio maeneo ambayo hata Gamondi aliweka bayana anahitaji maboresho
Okrah ni winga wakati Simon Msuva ambaye pia anahusishwa pamoja na Agee wanaweza kutumika kama winga au washambuliaji