Baada ya kuichapa Jamhuri Fc mabao 5-0 katika mchezo wa kwanza wa kombe la Mapinduzi, Yanga inashuka tena dimbani huko Zanzibar kuikabili Jamus ya Sudan Kusini ukiwa ni mchezo wa pili kundi C
Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe ametamba kuwa wataendeleza utaratibu ya kusimika 5G huko Zanzibar
"Tuliwaona Jamus katika mchezo wa waliopata sare dhidi ya KVZ, lakini nafikiri kesho (leo) wanakwenda kukutana na jambo zito pale New Amaan Complex," alisema Kamwe
Katika mchezo huo huenda Wananchi wakamshuhudia Maxi Nzengeli dimbani baada ya kocha Miguel Gamondi kumpumzisha katika mchezo uliopita
Mlinzi wa kushoto Nickson Kibabage aliyekuwa katika majukumu ya timu ya Taifa, amerejea baada ya kukosa nafasi kwenye kikosi cha mwisho cha Stars kilichosafiri kwenda Misri jana
Joyce Lomalisa nae yuko fit, jana akianza mazoezi na wenzake, pengine Gamondi anaweza kumrejesha uwanjani katika mchezo huo
Aidha winga Augustine Okrah aliyetambulishwa na Yanga juzi nae yuko fit pengine anaweza kupewa dakika chache kuwapa burudani Wananchi katika mchezo huo utakaopigwa saa 2:15 usiku