Mchezo wa tatu kundi C kombe la Mapinduzi kati ya Yanga dhidi ya KVZ umemalizika kwa matokeo ya suluhu ya bila kufungana
Ulikuwa mchezo wa kukamilisha ratiba kwa Yanga ambayo tayari ilikuwa imekata tiketi ya kutinga robo fainali
Mkufunzi wa Yanga Miguel Gamondi alifanya mabadiliko makubwa ya kikosi kilichoanza leo akiwaanzisha wachezaji 9 wa Yanga U20
Katika kipindi cha pili aliwaingiza Kibwana Shomari, Jesus Moloko, Joyce Lomalisa na Augustine Okrah ambaye hata hivyo alitolewa baada ya kuumia kichwani nafasi yake ikichukuliwa na Farid Mussa
ADVERTISE HERE