Mechi za hatua ya robo fainali kombe la Mapinduzi zinatarajiwa kuanza kutimua vumbi kesho Jumapili ambapo Yanga itachuana na APR ya Rwanda
Mchezo huo utapigwa saa 2:15 usiku katika uwanja wa New Amaan Complex
Mchezo wa kwanza wa robo fainali ni kati ya KVZ dhidi ya Mlandege ambao utapigwa Jumapili saa 10:15 jioni
Azam Fc na Singida FG zitachuana katika mchezo wa tatu wa robo fainali siku ya Jumatatu, saa 10:15 jioni na mchezo wa mwisho ni kati ya Jamhuri dhidi ya Simba siku ya Jumatatu saa 2:15 usiku
ADVERTISE HERE