Wakati kesho Jumapili Yanga ikitarajiwa kucheza mechi ya robo fainali ya kombe la Mapinduzi dhidi ya APR, wachezaji Pacome Zouzoua, Yao Kouassi na Khalid Aucho wanatarajia kutua visiwani Zanzibar kuongeza nguvu
Nyota hao hawakuwa sehemu ya kikosi cha kocha Miguel Gamondi ambacho kilifanikiwa kushinda mechi mbili na kutoka sare mechi moja katika hatua ya makundi na kutnga robo fainali huku wakiongoza kundi C
Pacome alikuwa Ivory Coast katika majukumu ya timu ya Taifa ambapo hata hivyo hakufanikiwa kupenya katika kikosi cha mwisho cha Ivory Coast kitakachoshiriki Afcon 2023


Yao na Aucho ni miongoni mwa wachezaji waliotumika sana msimu huu hivyo walipewa mapumziko na sasa wako tayari kurejea kikosini
ADVERTISE HERE