Kipaji kingine kilichoibuliwa Zanzibar

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Jan 2024
Kipaji kingine kilichoibuliwa Zanzibar

Yanga  iko jijini Dar es salaam wakitokea Zanzibar ambako safari yao kwenye kombe la Mapinduzi iliishia hatua ya robo fainali

Katika michuano hiyo, Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi aiamua kutumia kikosi cha vijana pamoja na wachezaji ambao hawakuwa wakipata nafasi katika kikosi cha kwanza

Ni uamuzi ambao haukuwafurahisha baadhi ya mashabiki hasa baada ya Yanga kuondoshwa katika michuano hiyo lakini kwa upande wa Gamondi ulikuwa uamuzi wenye malengo

Katika michuano hiyo baadhi ya wachezaji walipata nafasi ya kutosha kuonyesha uwezo wao na pengine huenda miongoni mwao wakaanza kuonekana katika timu ya kwanza

Miongoni mwa wachezaji hao ni kinda la U20, Khamis Nanguka ambaye alicheza katika safu ya ulinzi sambamba na Mganda Gift Fred

Nanguka alionyesha ukomavu katika michuano hiyo na pengine anaweza kupandishwa katika timu ya wakubwa ya Yanga

Kwa nyakati tofauti, Nanguka amejumuika kufanya mazoezi na timu ya wakubwa lakini hakuwa amepata nafasi ya kucheza mechi za ushindani

Gamondi amesema Nanguka ni miongoni mwa wachezaji waliomvutia katika michuano hiyo pengine Wananchi watarajie kumshuhudia zaidi katika kikosi chake

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
2h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
10h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’