Wakati dirisha dogo la usajili likitarajiwa kufungwa leo, huenda wananchi wakafunga usajili kwa utambulisho wa mshambuliaji mpya
Ni kutokana na mapendekezo ya mkufunzi wa Yanga Miguel Gamondi ambaye baada ya michuano ya kombe la Mapinduzi aliutaka uongozi kuhakikisha unasajili mshambuliaji kabla ya dirisha kufungwa
Siku chache zilizopita katika Harambee ya kuchangia timu za Taifa, Rais wa Yanga Injinia Hersi Said alifichua kuwa usajili haujakamilika na mchezaji mmoja atatambulishwa kabla ya dirisha kufungwa
"Bado hatujakamilisha usajili, tutamleta mchezaji mmoja kabla ya dirisha la usajili kufungwa," Hersi alisema
Mpaka sasa Yanga imekamilisha usajili wa wachezaji wawili Augustine Okrah na Shekhan Khamis na mchezaji anayesubiriwa huenda akawa mshambuliaji
Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kurejea mazoezini leo baada ya mapumziko ya wiki mbili