Nyota wa Yanga Stephane Aziz Ki na Djigui Diarra timu zao za taifa leo zinaanza kampeni ya kuwania taji la michuano ya Afcon 2023 inayoendelea huko Ivory Coast
Burkina Faso anayocheza Aziz Ki, itakuwa uwanjani saa 11 jioni kumenyana na Mauritania wakati Diarra na kikosi cha Mali watachuana na Afrika Kusin saa 5 usiku

Nyota wengine watano wa Yanga watashuka dimbani kesho katika mechi za timu za Taifa za Tanzania na Zambia
Tanzania itachuana na Morocco saa 2 usiku huku Zambia ikichuana na DR Congo saa 5 usiku
Bakari Nondo Mwamnyeto, Dickson Job, Ibrahim Bacca na Mudathir Yahya wako na timu ya Taifa ya Tanzania wakati Kennedy Musonda akiwa na timu ya Taifa ya Zambia
ADVERTISE HERE