Bacca anasaka heshima Ivory Coast

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Jan 2024
Bacca anasaka heshima Ivory Coast

Licha ya timu ya Taifa ya Tanzania kukubali kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Morocco katika mchezo wa kwanza wa michuano ya Afcon 2023 inayoendelea huko Ivory Coast, nyota wa Stars walipambana lakini uwezo wa Morocco pamoja na kadi nyekundu aliyopewa Novatus Dismas, ilikuwa sababu ya kipigo hicho

Safu ya ulinzi ya Stars iliongozwa na walinzi wawili wa Yanga Bakari Mwamnyeto na Ibrahim Hamad

Kama ni tuzo ya mchezaji bora wa mchezo kwa upande wa Stars, basi alistahili Bacca

Bacca ndiye mchezaji aliyehusika katika matukio mengi zaidi katika safu ya ulinzi pia akiwa kinara wa kupiga pasi

Bacca alishika nafasi ya pili kwa wachezaji waliopiga pasi nyingi katika mchezo huo nyuma ya beki wa Morocco Nayef Aguerd aliyepiga pasi 75 huku Bacca akipiga pasi 63. Sofyan Amrabat na Mwamnyeto wakifuata kila mmoja akipiga pasi 60

Katika mchezo huo Bacca aliondoa mipira 8 ya hatari, alipokonya mipira 8, mipira 5 aliondoa hatarini kwa kichwa, 'tackling' alifanya 5 na alishinda mipira 7 ya kugombania

Kwa hakika sasa Bacca ameiva! Yeye, Mwamnyeto na Job ni muhimili wa safu ya ulinzi ya Yanga na timu ya Taifa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
5h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
20h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’