Kikosi cha Yanga kinarejea leo jijini Dar es salaam kikitokea mkoani Singida kucheza mchezo wa robo fainali ya kombe la FA (ASFC).
Yanga imeondolewa kwenye mashindano hayo kwa mikwaju ya penati 4-2 baada ya matokeo ya sare ya bao 1-1 dhidi Singida United.
April 07 itashuka kwenye uwanja wa Taifa kuikabili Welayta Dicha katika mchezo wa kwanza wa kuwania nafasi ya kutinga hatua ya makundi kombe la Shirikisho Barani Afrika.
Yanga inarejea mapema ili kujiandaa na mchezo huo ambao ni lazima iibuke na ushindi nyumbani ili kuweka mazingira mazuri ya kutinga hatua ya makundi.
Uongozi wa Yanga umeuchukulia kwa umuhimu mkubwa mchezo huo na umekuwa ukiendelea na maandalizi hata kabla ya Yanga kuivaa Singida United jana.
Kocha Mkuu George Lwandamina alisafiri yeye mwenyewe kwenda nchini Ethiopia kuifanyia 'ushushushu' Welayta Dicha inayoshika nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi kuu ya Ethiopia.
Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amewataka mashabiki wa timu hiyo kusahau matokeo yaliyopita na waungane pamoja kuhakikisha Yanga inatinga hatua ya makundi kwa mara ya pili katika kipindi cha miaka mitatu.

ADVERTISE HERE