Mlinzi wa kati wa Yanga Gift Fred raia wa Uganda amepewa nafasi nyingine ya kupigania nafasi yake katika kikosi cha kwanza
Gift aliyetua Yanga katika dirisha kubwa la usajili lililopita akitokea SC Villa ya Uganda, alimanusra apewe mkono wa kwaheri katika usajili wa dirisha dogo
Hata hivyo kiwango alichoonyesha katika michuano ya kombe la Mapinduzi kikabadili upepo kwani Kocha Miguel Gamondi akapendekeza Mganda huyo aendelee kusalia katika kikosi chake
Ni wazi bado atakuwa na kazi ya kupigania nafasi yake mbele ya nahodha Bakari Nondo Mwamnyeto, Ibrahim Bacca na Dickson Job
Wakati yeye akiendelea na mazoezi Avic Town, wenzake wako kwenye majukumu ya timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' wakishiriki michuano ya Afcon 2023
Hatma ya Tanzania kuendelea kubaki Ivory Coast au kurejea nchini itaamuliwa kesho kwenye mchezo wa tatu hatua ya makundi dhidi ya DR Congo
Tanzania inahitaji kushinda mchezo huo ili kukata tiketi ya hatua ya mtoano