Hatma ya Ivory Coast kusonga mbele michuano ya Afcon 2023 itategemea na matokeo ya mechi zilizosalia hatua ya makundi zinazopigwa leo na kesho
Jana Ivory Coast ambao ni wenyeji wa michuano hiyo, walikubali kipigo cha mabao 4-0 kutoka kwa Guinea ya Ikweta wakishika nafasi ya tatu kundi A na alama tatu, wakifunga mabao 2 huku wenyewe wakiruhusu mabao 5
Ivory Coast wanategemea kuponea kupitia nafasi nne za 'best looser'
Katika mijadala iliyotawala katika kurasa za wadau wa soka nchini humo ni kiwango duni kilichoonyeshwa na timu yao huku wakihoji baadhi ya wachezaji kutojumuishwa katika kikosi cha timu hiyo
Kiungo mshambuliaji wa Yanga Pacome Zouzoua na nyota wa zamani wa Leiceste City Wilfred Zaha ni miongoni mwa majina yanayotajwa zaidi
Wachezaji wote walijumuishwa kwenye kikosi cha awali lakini wakaenguliwa kwenye orodha ya mwisho ya wachezaji 27
Kwa kiwango kilichoonyeshwa na timu yao, wengi wanaamini Pacome ambaye alikuwa mchezaji bora wa ligi kuu ya Ivory Coast msimu uliopita, alistahili kuwemo katika kikosi chao hasa kutoka na kiwango alichoonyesha kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika msimu huu
Pacome aliifungia Yanga mabao matatu katika michuano hiyo mabao mawili yakishinda tuzo ya goli bora la wiki. Katika Ligi ya NBC, Pacome ana mabao manne
Pacome yuko Avic Town akiendelea na mazoezi na kikosi cha Yanga akijinasibu kuwa pamoja na kuendelea kuiunga mkono timu yake ya Taifa, pia anaishangilia Taifa Stars