Stars yawekewa Bil 1.3 kuifunga DR Congo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Jan 2024
Stars yawekewa Bil 1.3 kuifunga DR Congo

Majira ya saa 5.00 usiku timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' itashuka katika Uwanja wa Amadou Gon Coulibaly mjini Karhogo kuchuana na DR Congo katika mchezo ambao utaamua hatma ya Stars kusonga mbele katika michuano ya Afcon 2023

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeweka mezani ahadi ya donge nono kwa wachezaji kama watashinda mchezo huo na kufuzu hatua ya mtoano

Taifa Stars inahitaji ushindi dhidi ya DR Congo ili kuwa na nafasi ya kufuzu hatua ya mtoano moja kwa moja au kupitia 'best looser'

Kwa sasa Stars ina pointi moja kundi F wakati Morocco ikiongoza na alama nne, DR Congo na Zambia zimekusanya pointi mbili kila moja.

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Damas Ndumbaro amesema TFF imetoa ahadi ya Tsh Bilioni 1.3 kwa ushindi wa Stars

Dk Ndumbaro amesema kuwa ahadi hiyo imewekwa ili kuwaongezea wachezaji hamasa na anaamini kuwa wachezaji watapambana mpaka tone la mwisho ili kushinda na kuiweka Tanzania katika ramani mpya ya soka

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’