Usiku wa kuamkia leo ilikuwa simanzi kwa mashabiki wa soka wa Tanzania baada ya kuishuhudia timu yao ikitupwa nje ya michuano ya Afcon 2023 ikilazimishwa suluhu ya bila kufungana dhidi ya DR Congo
Kwa upande mwingine matokeo hayo ni furaha kwa makocha wa klabu ambazo zilliwakosa wachezaji wengi kutokana na ushiriki wao katika michuano hiyo
Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi atafurahi kuwapokea wachezaji 5 waliokuwa Stars na Zambia
Bakari Nondo Mwamnyeto, Dickson Job, Ibrahim Bacca na Mudathir Yahya walikuwa kikosi cha Stars wakati Kennedy Musonda akiwa kikosi cha Zambia
Musonda jana alianza katika mchezo dhidi ya Morocco ambao hata hivyo walipoteza kwa bao 1-0 na kutupwa nje ya mashindano
Gamondi ataendelea kuwakosa nyota wawili Djigui Diarra na Stephane Aziz Ki ambao timu zao zimefuzu hatua ya 16 bora lakini bahati mbaya kwao ni kuwa mmoja kati yao ataondoka katika hatua inayofuata
Burkina Faso na Mali zitachuana katika hatua ya 16 bora mchezo utakaopigwa Januari 30 2024
