TPLB kutangaza tarehe ya Ligi kurejea

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Jan 2024
TPLB kutangaza tarehe ya Ligi kurejea

Bodi ya Ligi wakati wowote itatangaza kuendelea kwa ratiba baada ya timu za Taifa za Tanzania na Zambia kutolewa katika michuano ya Afcon 2023 inayoendelea huko Ivory Coast

Mtendaji Mkuu wa Bodi Almas Kasongo amesema wakati wowote kuanzia leo watatangaza tarehe ya ligi hiyo kurejea

Kasongo amesema kwa mujibu wa kanuni timu ambayo itakuwa na kuanzia wachezaji watatu katika timu ya Taifa, mechi zake zitasimama lakini kwa sasa hakuna timu ya ligi kuu ambayo ina wachezaji watatu au zaidi katika timu za Taifa

"Kama tulivosema toka awali, Ligi yetu itarejea rasmi pale tutakapokuwa tumerejea kutoka kwenye fainali za Afcon 2023, muhimu tunazingatia kanuni"

"Endapo klabu itakuwa na wachezaji wasiopungua watatu kwenye timu ya taifa maana yake michezo yake itasimama lakini kwa mazingira ambayo tunayo hulioni tena hilo"

"Kesho (leo) tutakaa kama Bodi kufanya majumuisho na kutangaza rasmi tarehe ya kurudi kwa Ligi Kuu ya NBC. Tunarudi vipi? tutarudi pale tulpoishia," alisema Kasongo

Yanga ina wachezaji wawili Stephane Aziz Ki na Djigui Diarra ambao bado wamebaki Ivory Coast baada ya Burkina Faso na Mali kutinga hatua ya 16 bora

Timu hizo zitachuana Januari 30 ambapo maana yake ni kuwa baada ya mchezo huo, mchezaji mmoja ataendelea hatua inayofuata huku mmoja akirejea Tanzania kuendelea na mikiki mikiki ya Ligi Kuu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18m ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
42m ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
8h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
14h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’