Bodi ya Ligi leo imetoa ratiba ya mechi za viporo. Kwa mujibu wa ratiba hiyo, Yanga itakuwa na wiki mbili za bandika bandua
Kesho Jumanne, mchezo wa kiporo kombe la FA dhidi ya Housing utapigwa katika uwanja wa Azam Complex
Februari 02 Yanga itakuwa mkoani Kagera kuumana na Kagera Sugar mchezo utakaopigwa saa 10 jioni
Februari 05 Yanga itakuwa uwanja wa Azam Complex kuumana na Dodoma Jiji katika mchezo utakaopigwa saa 1 usiku
Februari 08 Yanga watakuwa Azam Complex kuumana na Mashujaa katika mchezo utakaopigwa saa 1 usiku
Februari 11 Yanga watakuwa Mbeya kuumana na Tanzania Prisons
Februari 15 Yanga itaanza mechi za mzunguuko wa pili kwa kuumana na KMC katika mchezo ambao bado haujafahamika utachezwa katika uwanja gani






ADVERTISE HERE