Kesho Jumanne Yanga itashuka uwanja wa Azam Complex kuikabili Housing Fc katika mchezo wa raundi ya pili kombe la Shirikisho la Azam (ASFC)
Yanga itashuka dimbani kuikabili Housing Fc bila ya wachezaji wake waliokuwa katika majukumu ya timu za Taifa
Wakati Ibarahim Bacca, Bakari Mwamnyeto, Mudathir Yahya na Dickson Job wakiwa tayari wamerejea nchini kutoka Ivory Coast wakiwa na Stars, Yanga itawakosa kwa muda mrefu zaidi Stephane Aziz Ki na Djigui Diarra ambao timu zao za Taifa (Burkina Faso vs Mali) zitachuana kesho kuwania tiketi ya kutinga robo fainali Afcon 2023
Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amemuandaa nyota mpya Augustine Okrah kuziba pengo la Aziz Ki wakati wote ambao atakosekana
Katika mazoezi ya Yanga yanayoendelea Avic Town, Gamondi anawatumia pamoja Pacome Zouzoua, Maxi Nzengeli na Okrah hivyo Wananchi watarajie MAP itaendelea kama kawaida
Gamondi ameagiza wachezaji wote waliokuwa timu za Taifa wawe wameripoti kambini siku ya Jumatano kabla ya Yanga kuelekea Bukoba kuikabili Kagera Sugar mchezo wa Ligi Kuu Februari 02