Februari 02 Yanga itaendelea na kampeni ya kutetea ubingwa wa ligi kuu kwa mchezo dhidi ya Kagera Sugar ambao utapigwa katika uwanja wa Kaitaba
Habari njema kwa mashabiki wa Yanga ni kuwa kiungo Khalid Aucho atakuwa amemaliza adhabu ya kukosa mechi tatu hivyo atakuwa sehemu ya mchezo huo
Baada ya kupewa kadi nyekundu katika mchezo dhidi ya Coastal Union, Aucho alikosa mechi mbili za ligi dhidi ya Mtibwa Sugar na Tabora United na pia atakosa mchezo wa kombe la FA dhidi ya Housing siku ya kesho Jumanne
Aucho atarejea kikosini kwenye wakati mwafaka kwani Yanga inabaliwa mechi mfululizo za viporo katika kipndi cha wiki mbili
ADVERTISE HERE